Nahodha wa Timu ya taifa ya Wanawake, Twiga Stars Opah Clement ametambulishwa kwenye kikosi cha SD Eibar inayoshiriki Ligi Kuu Hispania maarufu Liga F.
Ametambulishwa kikosini hapo akitokea FC Juarez ya Mexico aliyoitumikia kwa msimu mmoja akicheza mechi sita kati bila ya kufunga bao wala asisti.
Nyota huyo wa kimaaifa wa Tanzania anakuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na timu inayoshiriki ligi hiyo ambayo inashika nafasi yapili kwa ubora barani Ulaya.