Mshambuliaji mpya wa Simba SC, Jonathan Sowah raia wa Ghana, amesema leo kwamba kila kombe ambalo Simba SC itashiriki lazima litue Msimhazi kutokana na maandalizi waliyonayo kwa sasa.
Sowah ameyasema baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam na timu yake ya Simba iliyokuwa kambini nchini Misri.
“Mashabiki wa Simba wasijali hata kama naikosa Ngao ya Jamii ila tutakutana nao kwenye Ligi hilo ndilo jambo la msingi, ndoto yetu ni kuleta kila kombe Msimbazi”
Amesema Jonathan Sowah, Mshambuliaji wa Simba SC