Dili la kiungo Ahmed Pipino kujiunga na klabu ya Simba SC limekufa ramsi baada ya Magnet Academy ambao wanammiliki mchezaji huyo kuhitaji kiasi cha pesa cha Tshs 200M ili auzwe kutoka KMC FC
Awali klabu ya KMC ilitaja kiasi cha Tshs 150M ili imuachie kiungo huyo huku Magnet Academy wakihimiza kuwa wao ndio wanamamlaka zaidi na kiungo huyo na thamani yake ni hiyo waliyoitaja na mpaka sasa Simba SC wamesitisha mauzo yake wakiamini kiungo huyo ana thamani ya Tshs 150M na ikiwa watatoa Tshs 200M ndio Magnet Academy watamuachia kiungo huyo.