Klabu ya Yanga Princess imemtambulisha kocha wake mpya wa utimamu wa mwili/viungo (fitness coach), Brenda Chaora raia wa Zimbabwe.
Brenda kabla ya kujiunga na Yanga Princess aliwahi kuwa kocha wa Fitness wa Simba Queens (timu ambayo iliyomtambulisha katika soka la Tanzania),kisha baadae akajiunga na Fountain Gate Princess na sasa amejiunga na Wananchi.
Ubora wake,taaluma,Uzoefu na Elimu yake ndio vitu bora zaidi na vya pekee vinavyotenga daraja lake na baadhi ya makocha wengi wa fitness hapa nchini.