Mabingwa watetezi wa Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Senegal wametupwa nje ya michuano hiyo kufuatia kipigo cha penalti 5-3 dhidi ya Morocco katika katika dimba la Mandela, Kampala.
Simba wa milima ya Atlas, Morocco wametinga fainali ya CHAN2024 ambapo watachuana na Madagascar iliyofikia hatua hiyo baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan. Simba wa Teranga watachuana na Sudan kuwania nafasi ya mshindi wa tatu.
Timu hizo ndani ya dakika 120 zilifungana 1-1 lakini mikwaju ya penalti ikatenganisha ambapo Senegal ikapata 3 na Morocco 5