Winga wa zamani wa Yanga SC, Jesus Moloko amejiunga na Klabu ya AS Kigali kwa mkataba wa Mwaka mmoja.
Moloko alikuwa kwenye kiwango bora alipokuwa katika klabu ya Yanga SC akiwa sambamba na mshambuliaji Fiston Mayele ambaye sasa yupo Pyramids.
Akiwa Yanga, Moloko aliisaidia kutwaa ubingwa wa bara misimu mitatu aliyokaa.