KLABU ya JKT Tanzania imeachana na Wachezaji wake wawili tegemeo wa safu ya ulinzi, kipa Yacoub Suleiman Ali (25) na beki Wilson Edwin Nangu (23) ambao wote wapo mbioni kujiunga na Simba SC.
Wawili hao wamekuwa wakitajwa katika taarifa za chanzo mbalimbali kuwa katika mazungumzo na Simba SC na taarifa hizi za JKT kuachana nao mara tu baada ya kumaliza majukumu hao katika timu ya taifa zinaashiria ukweli.
Yakoub amedaka mechi zote tano za timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Katika Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) ikitolewa katika hatua ya Robo Fainali akiruhusu mabao mawili tu.
Nangu bado ni beki wa benchi Taifa Stars ambaye kwa kipaji na juhudi zake anatabiriwa makubwa siku za usoni.
Yakoub amedumu kwa misimu miwili tu JKT Tanzania tangu awasili kutoka JKU ya Zanzibar, wakati Nangu ameichezea timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa msimu mmoja tu akitokea TMA Stars ya Arusha.