Kiungo mkabaji mpya wa Singida Black Stars, Khalid Aucho ameitwa kwa mara ya kwanza na timu ya taifa ya Uganda The Cranes tangu alipojiunga na klabu hiyo akitokea kwa mabingwa wa soka Tanzania bara, Yanga SC.
Aucho aliachana na Yanga baada ya kushindwana katika suala la kuongeza mkataba, hivyo kiroho safi Yanga walimpa thank you, lakini mabosi wa Singida Black Stars walipita naye.