Huenda Namungo inaenda kupata mwarobaini katika eneo lake la ushambuliaji ambalo msimu uliopita liliambulia kufunga mabao 28 tu katika #LigiKuu ,
Ongezeko la Rashid Mchelenga ambaye wamemnasa msimu huu kutoka Rwanda kunako klabu ya Musanze na Heritier Makambo kutoka Tabora united huenda likapunguza ufinyu wa upatikanaji wa mabao 2025/26.
Mchelenga ana uzoefu na soka la Tanzania ambapo aliwahi kuitumikia klabu ya Pamba Jiji aidha Lipuli ya Iringa hata nje ya Tanzania amezitumikia klabu za Police Kenya na Musanze ya Rwanda si jambo Dogo!
Rashid Mchelenga amerudi nyumbani kutoa ladha na hekaheka kwa wakazi wa Ruangwa na viunga vyake,