Klabu ya Simba SC imethibitisha kumsajili mshambuliaji Seleman Mwalimu ‘Gomez’ kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja akitokea Wydad Casablanca ya Morocco.
Mwalimu (19) raia wa Tanzania aliyejiunga na Wydad mnamo Januari 2025, akitokea Singida Black Stars baada ya kuonesha kiwango bora wakati akiitumikia Fountain Gate FC kwa mkopo kutoka Singida Black Stars na kufunga magoli 6 kwenye nusu ya kwanza ya msimu wa 2024/25.