Timu ya Yanga Princess haitaitangaza tena kampuni ya kubashiri SportPesa. Hii ni kutokana na uamuzi wa timu hiyo kutafuta mdhamini wake wa kujitegemea, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo udhamini wa timu ya wanaume ulihusisha pia timu ya wanawake.
Kuanzia sasa, wachezaji watakaotambulishwa hawatakuwa na tangazo lolote la SportPesa—iwe kwenye jezi za mazoezi, jezi za mechi, au mavazi yao mengine yote.
Yanga Princess sasa ipo kwenye mchakato wa kutafuta mdhamini mpya, na pia inakaribisha makampuni mbalimbali kujitangaza kupitia timu ya wanawake ya Yanga Princess.
Huu ni wakati wa mapinduzi—tuanze kuzipa thamani timu zetu za wanawake kwa kujitegemea katika udhamini, ili kuongeza hadhi yao na kupunguza mzigo wa kifedha ndani ya vilabu vyetu.