Taarifa zilizotufikia ni kwamba Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally anakuwa Mkurugenzi wa mashabiki wa klabu ya Simba SC na aliyekuwa msemaji wa Yanga SC, Haji Manara anarejea kuwa Meneja wa habari na mawasiliano wa klabu ya Simba SC.
Ahmed Ally tayari ameshaanza majukumu yake ya Ukurugenzi wa mashabiki na jana alikuwa Mafinga kukamilisha uzinduzi wa Simba Day, muda si mrefu Haji Manara anakwenda kutambulishwa kurejea kwenye nafasi yake.
Ikumbukwe Manara alipokuwa msemaji wa Simba, ikifanikiwa kushinda makombe yote ya Tanzania bara katika misimu minne mfululizo.
KARIBU Msimbazi Haji Manara