Mgombea wa Urais Kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi waliohudhuria uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika viwanja vya Tanganyika Packers Jijini Dar es Salaam tarehe 28 Agosti, 2025 ametoa ahadi zifuatazo katika siku zake 100 za kwanza akiwa madarakani;
✅ Marufuku kuzuia maiti hospitalini
✅ Bima ya Afya kwa Wazee, Watoto, Walemavu
✅ Wagonjwa wa saratani, sukari, figo kugharamiwa
✅ Wahudumu 5,000 wa afya kuajiriwa
✅ Walimu wapya 7,000 kuajiriwa
✅ Bilioni 200 kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo
✅ Kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya
✅ Mawaziri, wakuu wa mikoa kuwajibika kwa wananchi
✅ Kurasmisha sekta isiyo rasmi
✅ Kuanzisha Gridi ya Taifa ya Maji