Msanii wa muziki wa kizaxi kipya aliyewahi kuwa memba wa lebo za Yamoto Band na WCB, Mbwana Yusuf Kilungi "Mbosso" atapamba tamasha kubwa la klabu ya Simba la Simba Day siku ya Septemba 10 mwaka huu katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam.
Klabu ya Simba imeweka wazi hii leo kupitia msemaji wake Ahmed Ally ambapo Mbosso atakuwa jukwaa kuu akiwapa furaha mashabiki wa klabu hiyo.