Rais wa Young Africans SC, Injinia Hersi Said leo amemtembelea Katibu wa zamani wa Klabu yetu, Mzee Jabir Katundu na kumkabidhi zawadi za jezi zetu mpya za msimu wa 2025/26.
Mzee Jabir Katundu alikuwa Katibu wa Klabu ya Yanga miaka ya 1962-1966, chini ya Uongozi wa Mwenyekiti Mohamed Mabosti.
Hersi amemkabidhi Mzee Jarib Katundu, jezi zote za Klabu na kumuelezea maudhui yaliotumika kwenye ubunifu wa jezi hizo.