Afisa Habari wa Klabu ya Mlandege, Ally Mohamed amejiuzulu nafasi yake kuanzia leo Agosti 21, 2025.
Inatajwa kuwa Ally anatarajiwa kujiunga na klabu nyengine ya Ligi Kuu Zanzibar mwanzoni mwa msimu huu mpya.
Hatua hii inakuja, zikiwa zimesalia siku chache kuelekea michuano ya kimataifa ambapo Mlandege ipo katika maandalizi ya michuano hiyo.
Karibu miaka 2 imepita toka Ally alipojiunga na Mlandege kama Afisa habari wa klabu hiyo.