MSHAMBULIAJI Clement Francis Mzize ameongeza mkataba wa kuendelea kuitumikia Yanga – baada ya klabu yake kuposti picha akiwa na Rais wa timu, Eng Hersi Said na kuambatanisha na ujumbe “Bado yupo sana.
Mambo Uwanjani Blog ilikuwa ya kwanza kuwakilisha umma kwamba Mzize atabaki Yanga na sababu kubwa ni kumuongeza mkataba na kuboresha maslahi yake ambapo ilieleza kwamba Yanga itamlipa mshahara mkubwa ikitaja milioni arobaini na tano.