Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2025

Morice Abraham atambulishwa Simba

KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Morice Michael Abraham (21) kuwa mchezaji wake mpya baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Spartak Subotica ya Serbia. Abraham ni mchezaji aliyeibukia katika akademi ya Alliance ya Mwanza, kabla ya kwenda Spartak Subotica mwaka 2021 alikoanzia kucheza timu ya vijana, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa – na mwaka jana akapelekwa kwa mkopo RFK Novi Sad ya Serbia pia. Ikumbukwe jana Simba ilimtambulisha kiungo Msenegal, Alassane Maodo Kanté (24) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao akitokea CA Bizertin ya Tunisia. Kante ni mchezaji aliyeibukia katika klabu ya US Gorée ya kwao, Senegal mwaka 2019 kabla ya kwenda CA Bizertin mwaka 2022. Wanafanya idadi ya wachezaji wapya watatu waliotambulishwa rasmi Simba SC hadi sasa – baada ya beki wa kati wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck (29) anayeweza pia kucheza kama kiungo wa ulinzi pia kutoka Mamelodi Sundowns ya kwao. Lakini tayari imethib...

Ligi Kuu bara 2025/2026 kuanza kutumia vumbi Sept 16

MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, 2025/2026 unatarajiwa Septemba 16, mwaka huu 2025 – wastani wa wiki mbili tu baada ya kumalizika kwa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN). Msimu mpya wa Ligi Kuu umelazimika kuchelewa kutokana na Tanzania mwenyeji mwenza wa CHAN pamoja na jirani zake, Kenya na Uganda zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu. Ni kutokana na uenyeji wa CHAN tukio la utoaji Tuzo kwa nyota waliofanya vizuri msimu uliopita wa LIgi Kuu halijafanyika hadi sasa na pia haifahamiki kama michuano ya Nguo ya Jamii ambayo hushirikisha timu nne zilizomaliza nafasi za juu itakuwepo msimu huu. Timu 16 zinazotarajiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao ni pamoja na mabingwa watetezi, Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida Black Stars, Tabora United, Coastal Union, Mashujaa, Dodoma Jiji FC, JKT Tanzania, Namungo FC, KMC, Pamba Jiji, Tanzania Prisons, Fountain Gate, Mtibwa Sugar na Mbeya City. Katika CHAN Kundi A kuna Kenya, Morocco, Angola Jamhuri ya Kidemokrasi...

Oscar Mirambo aula CAF

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Oscar Mirambo ameteuliwa na CAF kuwa miongoni mwa Kundi la Wataalamu wa Ufundi wa CAF (Technical Study Group) katika mashindano ya CHAN na atakuwa kundI C ambalo litakuwa Uganda

SIMBA NAONA WANARUDIA YALE YALE YA MSIMU ULIOPITA

Na Prince Hoza DIRISHA kubwa la usajili la msimu uliopita klabu ya Simba SC ilifanya usajili mkubwa ambao ulitazamwa kama sehemu ya kujenga kikosi upya, ni kweli Simba ilianza kwa kumleta kocha mpya Fadlu David's raia wa Afrika Kusini. Lakini pia iliachana na wachezaji wake ambao wengine iliwasajili msimu juzi, kwa maana kwamba wachezaji ambao waliachwa msimu jana walisajiliwa msimu juzi, na hiyo yote imetokana na skauti mbaya iliyofanywa na waliokuwa wanasimamia usajili. Kumaliza kwenye nafasi ya tatu na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, kuliwafanya viongozi wa Simba kuamua kufumua kikosi na kusajili wachezaji wapya pamoja na Mkuu wa benchi la ufundi. Dirisha kubwa la msimu jana Simba ilifanya usajili mkubwa ambao ulipigiwa hesabu kwamba timu itakuwa moto wa kuotea mbali, ni kweli Simba waliamua kuweka kambi nchini Misri ambapo lengo nikuwapa maandalizi wachezaji wake. Na waliporudi kwenye ligi walianza vizuri na timu kurudisha matumaini kwa...

Kimenuka, Azam FC yaiburuza Yanga, TFF

Klabu ya Azam imeipeleka Yanga TFF kulalamikia kumtambulisha Mchezaji wao Abubakar Othman (Ninju) bila wao kuwa na taarifa yoyote . Ninju anamkataba na Azam Mpaka Mwaka 2027 lakini Mwezi wa kwanza alitolewa kwenda JKU kwa mkopo wa miezi sita mkopo ambao umeisha mwishoni mwa Msimu huu . Kabla ya kurudi Azam Ninju katambulishwa Yanga . Azam waliwasiliana na Jku lakini Jku wakasema Ninju walishamruhusu kurudi Azam kwani Mkataba wake wa mkopo ulikuwa umekwisha , ndipo Azam wakaamua kufungua mashtaka TFF kudai haki Yao kwa Ninju . . Ninju alitambulishwa Yanga jumapili ya juzi tarehe 27.

Masharti ya Max Nzengeli yambakisha Nkane Yanga

Max Nzengeli ndio amembakisha Dennis Nkane Jangwani. Sharti kubwa ambalo Max aliweka ili asaini mkataba mpya ni kwamba na Nkane nae abaki kwa muda huo huo wa miaka 2 ambao Yanga walipanga kumbakisha yeye. Tena aliwaambia viongozi kuwa yeye Nkane ndio aanze kusaini na Max akaupitia mkataba wake kuhakikisha vipengele vyote viko sawa. Ndio Nkane akasaini na kutangazwa mwanzo kisha Max nae akatia wino siku kadhaa baadae. Max alipojiunga na Yanga misimu miwili nyuma, Nkane ndio mchezaji alikuwa nae karibu na alimsaidia sana kuyajua mazingira ya huku na kuzoea maisha haraka ndani ya Yanga. Nkane alimfaa Max mwanzo, Max amelipa fadhila mwisho.

AUCHO AAGA YANGA

KIUNGO wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho (31) ameaga kwenye Yanga SC na kufurahia alioyovuna akiwa na timu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Aucho amewashukuru na kuwaaga Yanga akijivunia kushinda mataji na klabu hiyo na pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika – ikiwemo kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023. “Young Africans! Familia yangu pendwa, nataka kusema kwamba wakati umefika wa kufunga ukurasa usiosahaulika maishani mwangu. Zaidi ya misimu minne iliyopita nimepata uzoefu wa hisia kali, kufikia malengo ya ajabu na kujenga kumbukumbu isiyofutika nanyi nyote,”amesema Aucho.

Azam FC yakubali kumwachia Feitoto aende Simba

Afisa habari wa klabu ya Azam Fc Zakharia Zaka zakazi amesema “ Kama Feisal Salum Feitoto mwenyewe atazungumza kuwa hayupo tayri kuendelea na sisi hatuna shida tutamuacha afuate Mkataba unavyosema huku na sisi tukiendelea na mipango mengine…. Lakini hatuwezi kuja hadharani na kuwaambia yeye Mwenyewe Mchezaji atawaambia nini cha kufanya ili aweze kuununua Mkataba wake .

Vifaa vipya vyamiminika Simba

Kiungo Mshambuliaji Mohamed Bajaber amewasili nchini Tanzania kwaajili ya kujiunga na klabu ya Simba SC akitokea Kenya Police FC Mohamed Bajaber atasaini documents zote baada ya makubaliano binafsi na Simba SC kukamilika na Simba SC kumalizana na Kenya Police FC

Kante atambulishwa Msimbazi

KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo Msenegal, Alassane Maodo Kanté (24) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao akitokea CA Bizertin ya Tunisia. Kante ni mchezaji aliyeibukia katika klabu ya US Gorée ya kwao, Senegal mwaka 2019 kabla ya kwenda CA Bizertin mwaka 2022. Anakuwa mchezaji mpya wa pili kutambulishwa rasmi Simba SC baada ya beki wa kati wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck (29) anayeweza pia kucheza kama kiungo wa ulinzi pia kutoka Mamelodi Sundowns ya kwao. Lakini tayari imethibitika pia Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah kutoka Singida Black Stars.

Beki wa Simba atua Mbeya City

Klabu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kati Ibrahim Ame kama Mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mashujaa FC ya Kigoma. Ibrahim Ame unakuwa usajili wa kwanza kutangazwa na klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki Ligi kuu ya NBC. Ikumbukwe kuwa Ame amewahi kupita vilabu kadhaa nchini ikiwemo Coastal Union, Simba SC, KMC pamoja na Mtibwa Sugar.

Kinda wa Ngorongoro Heroes ajiunga KMC FC ya Maximo

Mchezaji na Mlinzi wa Kati wa timu ya taifa ya vijana (U-20) Ngorongoro Heroes, Ibrahim Nindi amejiunga na KMC FC akitokea Mashujaa FC ya Kigoma. Ibrahim Nindi aliwahi kupita kwenye timu za vijana za Simba Sports Club.

Singida Black Stars yaondolewa zuio la kusajili na FIFA

FIFA imewaondolea Singida Black Stars,adhabu ya kutosajili baada ya kulipa madeni yote ya wachazaji wao watatu. Awali Singida walikumbana na Rungu la FIFA baada ya kushindwa kulipa Stahiki za wachezaji wao watatu ambao ni Mbaraka Hamza,Amade Momade na Manu Bola. Ila kwa sasa Singida wako huru kusajili kwani kila kitu kimewekwa sawa

Feitoto kwenda Simba bure

Imefahamika kwamba kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum au Feitoto anatarajia kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Azam FC Ili aweze kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao. Ni ngumu kwa Feitoto kujiunga na Simba bila kuvunja mkataba kwa sababu Yanga SC wanataka walipwe bilioni 1 endapo mchezaji huyo akijiunga na Simba kwakuwa maelewano yao na Yanga wakati wanauziana ulieleza hivyo kwamba Feitoto akiuzwa kwa Simba basi Yanga watalipwa bilioni moja. Tayari mwanasheria wa Feitoto ameanza kuchukua hatua na muda wowote mkataba wake na Azam FC utavunjwa na itakuwa rahisi kujiunga na Simba bure pasipo kuilipa Yanga hata senti tano.

Rushine De Reuch ni Mwekundu wa Msimbazi

Rasmi klabu ya Simba imekamilisha usajili wa mlinzi wa zamani wa klabu ya Mamelodi Sundowns Rushine De Rueck kwa mkataba wa mwaka mmoja. Nyota huyo kabla ya kutua nchini alikuwa anaitumikia klabu ya Maccabi Petah ya nchini Israel kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns.

Simba na Betway imeishaa

KLABU ya Simba SC imepata udhamini mpya Mkuu kutoka Kampuni ya Betway Tanzania wenye thamani ya Sh. Bilioni 20 kwa miaka mitatu. Simba SC inaingia mkataba wa Betpawa baada ya kuachana na wadhamini wao, M-Bet walioingia nao mkataba wa miaka mitano kuanzia Agosti 1, mwaka 2022 wenye thamani ya Sh. Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000 kwa miaka mitano.

Injinia Hersi Said achinjiwa baharini ubunge Kigamboni

Chama Cha Mapinduzi(CCM) kimewateua Wagombea sita kugombea Ubunge Jimbo la Kigamboni akiwemo Ponela Matei, Habib Mchange, Allan Sanga, Henjelewe, Ally Mandai na Francis Elias. Rais wa Yanga Injinia Hersi Said jina lake halijarudi. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla ametangaza majina hayo leo Julai 29,2025.

Yanga yatambulisha wasaidizi wa kocha mkuu

KLABU ya Yanga imemtambulisha Mspaniola Alejandro Manu Rodríguez Lázaro (33) kuwa Kocha wake mpya chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz raia wa Afrika Kusini mwenye asili ya Morocco. Mzaliwa huyo wa Malaga anakuja kuungana na Folz ambaye amekwishafanya naye kazi katika timu kadhaa kwa nafasi hiyo hyo ya Usaidizi zikiwemo timu za vijana za Global Premier Soccer mwaka 2016, Antigua GFC U20, Juventud Canadiense FC, West Virginia na Chaos Guatemala. Manu Rodríguez pia amefanya kazi kama Kocha Msaidizi wa Randall Row raia wa Costa Rica katika timu za Ashanti Gold SC, Venezuela, Costa Rica U20, Costa Rica U20 Costa Rica U20 na U17. Aidha, Yanga pia imemtambulisha Muingereza, Paul Matthews kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Muafrka Kusini, Tshephang ‘Chyna’ Mokaila kuwa Kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili.

Minziro aashiwa taa ya kijani Pamba Jiji

Uongozi wa klabu ya Pamba Jiji Fc umetangaza kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Fredy Felix Minziro kwa makubaliano ya pande zote mbili. Taarifa ya leo Julai 28, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa klabu inaendelea na mchakato wa kumtafuta na kumtangaza kocha mkuu pamoja na msaidizi wake. “Uongozi umetoa shukrani za kipekee kwa kocha Minziro na benchi zima la ufundi, na umemtakia mafanikio mema ya soka nje ya Pamba Jiji.”— imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Imeisha....Maximo atambulishwa KMC

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Marcio Maximo ametambulishwa kama kocha mkuu mpya wa klabu ya KMC FC akichukua mikoba ya Kally Ongala aliyetupiwa virago mwezi Mei kutokana na mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo. Maximo (63) raia wa Brazil ambaye pia amewahi kuinoa Young Africans Sc anakumbukwa zaidi kwa kuiwezesha Taifa Stars kufuzu Michuano ya CHAN kwa mara ya kwanza mwaka 2009.

Dili la Feitoto kwenda Simba limekufa kisa Yanga

Inasemekana dili la kiungo mshambuliaji wa Azam FC na timu ya taifa, Taifa Stars, Feisal Salum au Feitoto kujiunga na Simba linaelekea kufeli baada ya Afisa Hahari wa Azam FC, Zakharia Zaka Zakazi kuweka wazi kila kitu kwamba Simba haiwezi kumnunua. "Azam haiwezi kumuuza Feisal kwenda Simba sababu Simba hiyo Pesa hawana, labda nikuambie mkataba wa Feisal unakipengele kama atauzwa kwenda Simba basi Yanga inabidi alipwe bilioni Moja (Yaani kwenye mkataba imetajwa kabisa Simba), sasa Simba atatoa shilingi ngapi ili Azam imlipe Yanga Bilion Moja na Azam abakiwe na Hela" . "Ndio maana nasema Simba hiyo Hela hawana labda waje na bilioni Mbili na nusu ili Yanga apewe bilioni Moja halafu Azam abakiwe na Bilion Moja na nusu sababu huwezi kuilipa Yanga Bilion Moja halafu sisi tubakiwe na Hela ndogo au tusipate Hela lazima sisi tupate Hela kubwa zaidi" . "Biashara ya Azam na Simba juu ya Feisal Haiwezi kufanyika yaani timu iliyonunuliwa kwa Bilion 20 unavyoona inaweza ku...

Valentino Mashaka atua Mbeya City

Mshambuliaji Valentino Mashaka amejiunga na klabu ya Mbeya City FC akitokea klabu ya Simba SC Valentino Mashaka amejiunga na Mbeya City kwa mkataba wa mwaka mmoja wa mkopo.

KMC kuweka kambi Zanzibar, Maximo ndani ya nyumba

Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu ya Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo anatarajia kuwasili nchini kwa ajili ya kujiunga na timu ya KMC ya Kinondoni. Maximo baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, ataungana na wachezaji wa timu hiyo kuelekea Zanzibar ambapo wataweka kambi. Maximo ataungana na kocha wake msaidizi, kwa vyovyote ushindani kwenye ligi yetu msimu ujao utakuwa mkubwa sana kutokana na uwepo wa makocha wakubwa.

Israel Mwenda asaini miaka mitatu Yanga

Beki wa timu ya Taifa la Tanzania Israel Patrick Mwenda amesaini mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Young Africans baada ya makubaliano ya pande zote tatu. (Singida Black Stars, Young Africans na Mchezaji mwenyewe). Mwenda sasa atawatumikia wananchi kwa muda wa miaka mitatu kuanzia msimu ujao mpaka 2028. Yanga wanaimarisha kikosi chao licha ya kuwa na Yao Atohoula na Kibwana Shomari ambapo pia wanaweza kucheza katika eneo hilo. Mwenda aliwahi kupita kunako vilabu vya Simba Sc, KMC na Singida Black Stars.

Najuta kuchezea Yanga - Baleke

Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Jean Baleke, amefunguka na kusema wazi kuwa anajutia uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo, huku akidai kuwa chaguo lake la kwanza alipoondoka Simba, lilikuwa ni Azam FC. : Baleke amesema kuwa wakati anafanya maamuzi ya mustakabali wake kisoka, moyo wake ulikuwa unamtuma kwenda Azam kutokana na mazingira na maono ya timu hiyo, lakini hali ya ushawishi kutoka Yanga yalimvuta na kumfanya abadili maamuzi. : “Nikikumbuka namna mambo yalivyokwenda, najuta. Azam walikuwa na mpango mzuri na walinionesha heshima ya kipekee, lakini nilishawishiwa kwenda Yanga na sasa naona sikufanya maamuzi sahihi,” alisema Baleke. : Kwa sasa haijafahamika wazi Baleke atatua wapi baada ya kuachana na Yanga, lakini taarifa zinadai kuwa Azam bado wanaweza kuwa na nia ya kumrejesha mezani kwa mazungumzo.

JS Kabylie kumng' oa Ahoua Simba

Klabu ya JS Kabylie imetuma ofa rasmi ya USD 600,000 (Tshs Bilioni 1.5) ili kupata saini ya Kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Jean Charles Ahoua kuelekea msimu ujao Simba SC wanaipitia ofa hiyo na ikiwalidhisha watamuuza kiungo Jean Charles Ahoua ambaye amekuwa na msimu bora sana.

Taifa Stars mabingwa wa CECAFA

TIMU ya taifa ya Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ katika mchezo wa mwisho wa michuano maalum ya Baraza la Vyama Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) jioni ya leo Uwanja wa Karatu, Karatu Jijini Arusha. Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Azam FC Abdul Suleiman Hamisi ‘Sopu’ dakika ya 52 na beki Ibrahim Hamad Abdullah ‘Bacca’ wa Yanga SC dakika ya 56 baada ya mshambuliaji wa AS Kaffrine, Mapathé Mbodji kuanza kwafungia Simba wa Teranga dakika ya nane. Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inakuwa mshindi wa jumla wa michuano hiyo kufuatia kuifunga na Uganda ‘The Cranes’ 1-0 katika mchezo wa kwanza, timu hiyo iliichapa Senegal 2-1 nayo kwenye mchezo wake wa kwanza hapo hapo Uwanja wa Karatu.

Simba yatenga bilioni 1.2 kumnunua Feitoto

Klabu ya Simba SC ipo tayari kutoa kiasi cha pesa cha USD 500K (Tshs Bilioni 1.2) kwenda Azam FC lakini italipa nusu yake USD 250K (Tshs Milioni 630) na nyingine watalipa baadae Azam FC wamekataa wanahitaji kiasi chote na bila hivyo hakuna biashara na Simba SC kwa Feitoto na mpaka sasa klabu ya Simba SC inaendelea kupambana kwa kuishawishi Azam FC ili ikubaliane na mahitaji hayo na Kiungo Feisal ameshasema yes kujiunga na Simba SC na anahitaji kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.

Singida Black Stars yaridhia Sowah kwenda Simba

MSHAMBULIAJI Mghana, Jonathan Sowah (26) amejiunga na Simba SC akitokea Singida Black Stars alikodumu kwa nusu msimu tangu awasili. Taarifa ya Singida Black Stars leo imesema kwamba wameridhia kumruhusu Sowah kujiunga na Simba SC baada ya mazungumzo baina ya watu wenye mamlaka ya juu kwenye timu zote. Hao ni Mlezi wa Singida Black Stars, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohamed Gulam ‘Mo’ Dewji ambaye pia ni Rais wa heshima wa klabu hiyo. Sowah alijiunga na Singida Black Stars Januari 17, mwaka huu 2025 akitokea Al-Nasr ya Libya ambako alidumu kwa msimu mmoja baada ya kuwasili akitokea Medeama ya kwao, Ghana Januari 27, mwaka jana 2024. Kisoka, haswa Sowah aliibukia Danbort FC ya kwao pia, Ghana kabla ya kuhamia Medeama SC Novemba 11, mwaka juzi, 2023. Akiwa Medeama ndipo Watanzania walianza kumuona mchezaji huyo kufuatia klabu yake hiyo kukutana na Yanga ambao ni wapinzani...

Hatimaye Yanga yamtambulisha mbadala wa Feitoto

KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Nizar Abubakar Othman ‘Ninju’ kutoka JKU ya Zanzibar kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao. Anakuwa mchezaji mpya wa tano Yanga SC na wa pili tu wa kigeni baada ya viungo Lassine Kouma kutoka Stade Malien ya kwao, Mali na Mguinea, Balla Mousa Conte kutoka CS Sfaxien ya Tunisia. Wengine ni wazawa wawili kiungo Abdulnasir Mohamed Abdallah kutoka Mlandege ya Zanzibar na winga Offen Francis Chikola kutoka Tabora United. Aidha, Yanga pia imeajiri kocha mpya Mkuu, Mfaransa Romain Folz mwenye asili ya Morocco ambaye amekuja na Msaidizi mmoja, Kocha wa Makipa. Majdi Mnasria.

Albamu yangu ya NJE NDANI nilifanya nje ya nchi- Mr Sugu

"Albamu yangu ya NJE YA BONGO nilifanyia Nje ya nchi mwaka 1999, na ndio albamu yangu ya kwanza kuisambaza mwenyewe. Big up kwa Mzee Kitime maana ndiye alinisaidia kusambaza albam yangu ya kwanza kabla ya albamu ya pili na ya tatu hazijachukuliwa na promota Mutta. Baada ya kutoridhika na mwenendo mzima wa biashara niliamua kuisambaza mwenyewe. Sasa, nikiangalia kila wanao-duplicate (durufu) ni wadosi, mahali pekee ambapo ningeweza ku-duplicate ni CHAMUDATA (Chama cha Muziki wa Dansi Tanzania) Wao walikuwa na sponsorship kutoka Norway chini ya Mzee John Kitime akiwa kama Katibu, pale walikuwa na studio na chumba kwa ajili ya ku-duplicate tapes. Nilimfuata Mzee Kitime nikamwomba ni-duplicate albamu yangu, akasema b'ana ili uwe mnufaika lazima uwe member. Wakati huo hatukuwa na Chama cha Rap ilibidi mimi niwe Mwanachama wa CHAMUDATA! Kwa hiyo, mimi nimewahi kuwa member wa CHAMUDATA, big up kwa brother Kitime kwa sababu yote hii alikuwa anatafuta namna ya kunisaidia." Joseph...

Tshabalala kocha mpya Sporting Club

Aliyekuwa kocha wa wanawake wa Mamelodi Sundowns Jerry Tshabalala ndiye kocha mkuu mpya wa Sporting Club Casablanca. Casablanca wanaoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini Morocco na walimaliza wa pili katika Ligi ya Mabingwa ya CAF ya Wanawake 2023 baada ya kushindwa na Sundowns ya Tshabalala.

Thapelo Maseko aota mbawa Simba

Mshambuliaji Thapelo Maseko hatajiunga na klabu ya Simba SC kuelekea msimu ujao akitokea Mamelodi Sundowns Pia Orlando Pirates imekataa ofa ya Simba SC ya kuhitaji kupata saini ya Karim Kimvuidi na wamemuahidi mchezaji atapewa muda wa kucheza kuelekea msimu ujao.

Salehe Karabaka arejea Simba

Mshambuliaji wa Klabu ya Simba SC, Salehe Karabaka , ambae alikuwa Kwa mkopo kwenye Klabu ya Namungo FC Kwa mwaka mmoja ambao tayari umemalizika amerejea katika Klabu ya Simba SC baada ya mkataba wake kufika mwisho. Mkataba wa Karabaka na Klabu ya Simba SC ni Miaka mitatu , mpaka sasa Simba ndo wataamua Nini wakifanye kama mchezaji atatokewa Kwa mkopo ama watasalia katika Klabu hiyo ya Msimbazi.

Yanga yatwaa kombe lingine mchangani

TIMU ya Yanga SC imetwaa Kombe la Safari Lager baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kombaini ya Safari Lager jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Bao pekee la Yanga ambayo ilitumia kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kikiongezewa nguvu na wachezaji watano wa akiba wa timu ya kwanza limefungwa na mshambuliaji Hemed Awam (18) dakika ya 22. Wachezaji wa akiba wa Yanga waliooingezea nguvu U20 yao chini ya kocha Vincent Barnabas ni kipa Abdutwalib Mshery, mabeki Kibwana Shomari na Nickson Kibabage, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mawinga Denis Nkane na Farid Mussa.

Moalin kwishinei Yanga

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Kocha Msaidizi wa Klabu ya Yanga Sc Abdulhamid Moalin hatokuwa sehemu ya kikosi cha Mabingwa hao wa Ligi Kuu bara msimu wa 2024/26 baada ya mkataba na waajiri wake hao kufikia ukomo. Moalin ambaye alijiunga na Yanga akitokea KMC katikati ya msim uliopita ameujulisha uongozi wa Yanga juu ya dhamira yake ya kutoongeza mkataba huku klabu hiyo ikibariki matakwa hayo baada ya kocha mpya Romain Folz kuhitaji kuwa na benchi lake binafsi. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Moalin na aliyekuwa mchambuzi wa video (video analyst) wanatarajiwa kujiunga na aliyekuwa kocha wa Yanga Sc Sead Ramovic kunako klabu ya CR Belouzidad.

Lassine Kouma atambulishwa Yanga

KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo chipukizi wa Kimataifa wa Mali, Lassine Kouma (21) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao 2025-2026. Kouma anasaini mkataba wa kujiunga na mabingwa wa Tanzania akitokea Stade Malien ya kwao, Bamako. Kouma ni mchezaji anayeweza kucheza kama kiungo wa ulinzi, winga, kiungo wa katikati, kiungo mshambuliaji na mshambuliaji wa katikati. Anakuwa mchezaji mpya wa nne Yanga SC na wa pili tu wa kigeni baada ya kiungo mwingine wa Kimataifa wa Guinea, Balla Mousa Conte kutoka CS Sfaxien ya Tunisia. Wengine ni wazawa wawili kiungo Abdulnasir Mohamed Abdallah kutoka Mlandege ya Zanzibar na winga Offen Francis Chikola kutoka Tabora United. Aisha, Yanga pia imeajiri kocha mpya Mkuu, Mfaransa Romain Folz mwenye asili ya Morocco ambaye amekuja na Msaidizi mmoja, Kocha wa Makipa. Majdi Mnasria.

Kakolanya mbioni kutua Mbeya City

Aliyewahi kuwa mlinda mlango wa Tanzania Prisons,Young Africans,Simba,Fountain gates (Zamani Singida Fountain gates) na Namungo,Beno Kakolanya anatajwa kuwa katika mipango ya Mbeya City kuelekea msimu 2025/26. Beno ni miongoni mwa walinda milango bora kuwahi kutokea aliwahi kuwa sehemu ya kikosi cha Tanzania katika michuano ya AFCON 2023 iliyofanyika Ivory Coast.

Ayoub Lakred aiponza Simba, FIFA

Taarifa zinasema kuwa Simba SC imefungiwa kusajili na FIFA, Ayoub Lakred alivunjiwa mkataba bila kulipwa stahiki zake ambazo ni $100,000 (Tsh 257,000,000) na FIFA wametoa adhabu hiyo na hawataruhusiwa kusajili au kutambulisha mchezaji mpya hadi deni hilo lilipwe. Simba wapo kwenye mchakato huo ili waweze kutangaza usajili mpya. FIFA wametuma taarifa hii siku kadhaa zilizopita ila ikawekwa kuwa siri.

Anaandika Hans Raphael, Fadlu anataka makombe

Baada ya kufungwa na Yanga 2-0 kwenye mechi ya mwisho ya ligi,Fadlu alisema Simba inakosa wachezaji wenye uwezo,uzoefu na mentality ya kucheza mechi kubwa na ngumu. Baada ya hapo alipeleka ripoti na kuwataka viongozi wa Simba wamuachie jukumu zima la kusajili…..viongozi wamekubali na kocha kaanza kushusha vyuma. Ukitazama usajili wa Fadlu hadi sasa utagundua vitu viwili vikubwa. 1. Anasajili wachezaji wenye uzoefu. 2. Anasajili wachezaji ambao anawafahamu. Ukitazama usajili wa Fadlu utagundua jamaa anahitahi watu wa kazi “Ready-made” ambao wamecheza mechi nyingi zenye pressure,Fadlu hataki kujaribu kwa vijana wadogo anataka watu wenye uzoefu ili waje kupiga kazi siyo kujifunza. Mfano Rushine De Reuck ana miaka 29,Neo Maema ana miaka (29),Jonathan Sowah (25),Khadim Diaw (26) na Alassane Kanté (24). Guys hapo hakuna mtoto,hao wote wana uzoefu wa kucheza ligi kubwa Africa. Lakini wengi wao Fadlu amewahi kufanya nao kazi na wengine kama Sowah anawafahamu kwani msimu jana alicheza dhidi yao...

Simba hawataki utani, yabeba Mzauzi mwingine wa Mamelodi

Klabu ya Simba imekamilisha kuinasa saini ya beki wa kati wa Mamelodi Sundowns, Rushine De Reuck mwenye umri wa miaka Ishirini na tisa (29) kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine endapo atafanya vizuri na kikosi cha Simba. . Rushine De Ruck alijiunga rasmi na Mamelodi Sundowns mwaka 2021, akitumikia misimu kadhaa kabla ya kwenda kujiunga Maccabi Petah Tikva ya Israel kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns. . Rushine De Reuck amewahi kufundishwa na kocha Fadlu Davids kipindi ambacho akiwa Martizbug United mwaka 2021 nchini Afrika Kusini, jambo ambalo limemshawishi kuja Simba baada ya kutambua uwepo wa Fadlu Davids. . Rushine De Reuck ndiye beki anayekuja kuziba nafasi ya Che Malone Fondoh katika safu ya ulinzi kwenye kikosi cha Simba SC

Rais wa FIFA aipongeza Yanga

Rais wa Shirikisho la soka ulimwenguni, FIFA, Gian Infatinho ameipongeza klabu ya Yanga SC ya Tanzania kwa kufanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu bara. Infatinho ametuma salamu zake kwa Yanga SC ikiwa ni desturi kwa Rais wa soka ulimwenguni kuzitumia salamu ya pongezi kwa timu bingwa wa nchi mwanachama wa Shirikisho hilo.

Simon Msuva akomaa Iraq

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Happygod Msuva (31) amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea klabu ya Al-Talaba SC ya Iraq. Taarifa ya Al-Talaba, klabu yenye maskani yake mjini Al-Rusafa Jijini Baghdad imesema kwa kifupi mno; “Mtanzania Simon Masova amesaini mkataba mpya,”. Msuva alijiunga na washindi hao wa mataji matano ya Ligi Kuu ya Iraq ‘Iraq Stars League’ Mei 8 mwaka 2024 akitokea Al-Najma ya Saudi Arabia ambako alicheza kwa nusu msimu akitokea JS Kabylie ya Algeria iliyomsajili Desemba 19 mwaka 2023. Msuva aliwasili JS Kabylie akitokea Al-Qadsiah ya Saudi Arabia aliyojiunga nayo Agosti 28 mwaka 2023 baada ya kuondoka Wydad Athletic ya Morocco aliyojiunga nayo Julai 24 mwaka 2022. Difaa El Jadida ndio klabu iliyomtambulisha Msuva katika soka ya Morocco baada ya kumsajili OKtoba 11, mwaka 2020 kutoka Yanga ya nyumbani, Dar es Salaam.

Simba yashusha beki mwingine wa kushoto

Klabu ya Simba SC imekamilisha usajili wa Mlinzi wa Kushoto, Miraji Abdallah Zambo Jr, kutoka Klabu ya Coastal Union. Nyota huyo alikuwa na Kiwango cha kuvutia sana akiwa na Klabu ya Wanamangishi ambao amewaaga msimu uliotamatika , sasa miraji anakwenda kuchukua nafasi ya Mohamed ambae ameondoka Klabuni hapo.

Mpanzu kimeeleweka Simba, sasa kujiunga na timu wiki ijayo

Kwa mujibu wa AJ vainqueur ambao ni wasimamizi wa Winga Elie Mpanzu wameeleza kuwa klabu ya Simba SC imelipa kiasi kilichokuwa kimebaki cha Tshs 190M na proposal zote za ada ya usajili Elie Mpanzu anajiandaa kurudi Tanzania kwaajili ya kuitumikia klabu ya Simba SC kuelekea msimu mpya na atafika jioni ya leo na bado ana mkataba na Wekundu wa Msimbazi.

Kinda wa Ngorongoro Heroes kucheza Ligi Kuu Sweden

Kinda wa kimataifa wa Tanzania,Sabri Kondo (17) yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga mazima na klabu ya ligi kuu ya Sweden BK Häcken. Awali klabu hiyo ilimualika Kondo kwenye majaribio na baada ya kumtazama kwa kina wameridhishwa na kiwango chake hivyo wamekubali kutoa €120,000 (tsh 361,632,000) kwenda Singida kama ada ya uhamisho wake. Msimu uliopita Kondo alicheza Coastal Union kwa mkopo akitokea Singida Black Stars.