MSIMU mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, 2025/2026 unatarajiwa Septemba 16, mwaka huu 2025 – wastani wa wiki mbili tu baada ya kumalizika kwa na Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN).
Msimu mpya wa Ligi Kuu umelazimika kuchelewa kutokana na Tanzania mwenyeji mwenza wa CHAN pamoja na jirani zake, Kenya na Uganda zinazotarajiwa kuanza Agosti 2 hadi 30, mwaka huu.
Ni kutokana na uenyeji wa CHAN tukio la utoaji Tuzo kwa nyota waliofanya vizuri msimu uliopita wa LIgi Kuu halijafanyika hadi sasa na pia haifahamiki kama michuano ya Nguo ya Jamii ambayo hushirikisha timu nne zilizomaliza nafasi za juu itakuwepo msimu huu.
Timu 16 zinazotarajiwa kushiriki Ligi Kuu msimu ujao ni pamoja na mabingwa watetezi, Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida Black Stars, Tabora United, Coastal Union, Mashujaa, Dodoma Jiji FC, JKT Tanzania, Namungo FC, KMC, Pamba Jiji, Tanzania Prisons, Fountain Gate, Mtibwa Sugar na Mbeya City.
Katika CHAN Kundi A kuna Kenya, Morocco, Angola Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Zambia, Kundi B kuna Tanznaia, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), wakati Kundi C linazikutanisha Uganda, Niger,
Guinea, Algeria na Afrika Kusini wakati Kundi D kuna Senegal, Kongo-Brazaville, Sudan na Nigeria.
Mechi za Kundi zitachezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Kundi B zitachezwa viwanja vya Nyayo na Moi Jijini Nairobi, Kenya, Kundi C Uwanja wa Mandela Jijini Kampala, Uganda na Kundi D Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.