TIMU ya Yanga SC imetwaa Kombe la Safari Lager baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kombaini ya Safari Lager jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Bao pekee la Yanga ambayo ilitumia kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kikiongezewa nguvu na wachezaji watano wa akiba wa timu ya kwanza limefungwa na mshambuliaji Hemed Awam (18) dakika ya 22.
Wachezaji wa akiba wa Yanga waliooingezea nguvu U20 yao chini ya kocha Vincent Barnabas ni kipa Abdutwalib Mshery, mabeki Kibwana Shomari na Nickson Kibabage, kiungo Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na mawinga Denis Nkane na Farid Mussa.