Max Nzengeli ndio amembakisha Dennis Nkane Jangwani. Sharti kubwa ambalo Max aliweka ili asaini mkataba mpya ni kwamba na Nkane nae abaki kwa muda huo huo wa miaka 2 ambao Yanga walipanga kumbakisha yeye.
Tena aliwaambia viongozi kuwa yeye Nkane ndio aanze kusaini na Max akaupitia mkataba wake kuhakikisha vipengele vyote viko sawa. Ndio Nkane akasaini na kutangazwa mwanzo kisha Max nae akatia wino siku kadhaa baadae.
Max alipojiunga na Yanga misimu miwili nyuma, Nkane ndio mchezaji alikuwa nae karibu na alimsaidia sana kuyajua mazingira ya huku na kuzoea maisha haraka ndani ya Yanga. Nkane alimfaa Max mwanzo, Max amelipa fadhila mwisho.