Kinda wa kimataifa wa Tanzania,Sabri Kondo (17) yuko kwenye hatua za mwisho za kujiunga mazima na klabu ya ligi kuu ya Sweden BK Häcken.
Awali klabu hiyo ilimualika Kondo kwenye majaribio na baada ya kumtazama kwa kina wameridhishwa na kiwango chake hivyo wamekubali kutoa €120,000 (tsh 361,632,000) kwenda Singida kama ada ya uhamisho wake.
Msimu uliopita Kondo alicheza Coastal Union kwa mkopo akitokea Singida Black Stars.