KLABU ya Yanga imemtambulisha Mspaniola Alejandro Manu Rodríguez Lázaro (33) kuwa Kocha wake mpya chini ya Kocha Mkuu, Romain Folz raia wa Afrika Kusini mwenye asili ya Morocco.
Mzaliwa huyo wa Malaga anakuja kuungana na Folz ambaye amekwishafanya naye kazi katika timu kadhaa kwa nafasi hiyo hyo ya Usaidizi zikiwemo timu za vijana za Global Premier Soccer mwaka 2016, Antigua GFC U20, Juventud Canadiense FC, West Virginia na Chaos Guatemala.
Manu Rodríguez pia amefanya kazi kama Kocha Msaidizi wa Randall Row raia wa Costa Rica katika timu za Ashanti Gold SC, Venezuela, Costa Rica U20, Costa Rica U20 Costa Rica U20 na U17.
Aidha, Yanga pia imemtambulisha Muingereza, Paul Matthews kuwa Mkurugenzi wa Ufundi na Muafrka Kusini, Tshephang ‘Chyna’ Mokaila kuwa Kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili.