Klabu ya Mbeya City ya mkoani Mbeya imetangaza kukamilisha usajili wa beki wa kati Ibrahim Ame kama Mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na Mashujaa FC ya Kigoma.
Ibrahim Ame unakuwa usajili wa kwanza kutangazwa na klabu hiyo ambayo msimu ujao itashiriki Ligi kuu ya NBC.
Ikumbukwe kuwa Ame amewahi kupita vilabu kadhaa nchini ikiwemo Coastal Union, Simba SC, KMC pamoja na Mtibwa Sugar.