Uongozi wa klabu ya Pamba Jiji Fc umetangaza kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Fredy Felix Minziro kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Taarifa ya leo Julai 28, 2025 iliyotolewa na klabu hiyo imebainisha kuwa klabu inaendelea na mchakato wa kumtafuta na kumtangaza kocha mkuu pamoja na msaidizi wake.
“Uongozi umetoa shukrani za kipekee kwa kocha Minziro na benchi zima la ufundi, na umemtakia mafanikio mema ya soka nje ya Pamba Jiji.”— imesema sehemu ya taarifa hiyo.