Klabu ya Simba imekamilisha kuinasa saini ya beki wa kati wa Mamelodi Sundowns, Rushine De Reuck mwenye umri wa miaka Ishirini na tisa (29) kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza mwaka mwingine endapo atafanya vizuri na kikosi cha Simba.
.
Rushine De Ruck alijiunga rasmi na Mamelodi Sundowns mwaka 2021, akitumikia misimu kadhaa kabla ya kwenda kujiunga Maccabi Petah Tikva ya Israel kwa mkopo akitokea Mamelodi Sundowns.
.
Rushine De Reuck amewahi kufundishwa na kocha Fadlu Davids kipindi ambacho akiwa Martizbug United mwaka 2021 nchini Afrika Kusini, jambo ambalo limemshawishi kuja Simba baada ya kutambua uwepo wa Fadlu Davids.
.
Rushine De Reuck ndiye beki anayekuja kuziba nafasi ya Che Malone Fondoh katika safu ya ulinzi kwenye kikosi cha Simba SC