Baada ya kufungwa na Yanga 2-0 kwenye mechi ya mwisho ya ligi,Fadlu alisema Simba inakosa wachezaji wenye uwezo,uzoefu na mentality ya kucheza mechi kubwa na ngumu.
Baada ya hapo alipeleka ripoti na kuwataka viongozi wa Simba wamuachie jukumu zima la kusajili…..viongozi wamekubali na kocha kaanza kushusha vyuma.
Ukitazama usajili wa Fadlu hadi sasa utagundua vitu viwili vikubwa.
1. Anasajili wachezaji wenye uzoefu.
2. Anasajili wachezaji ambao anawafahamu.
Ukitazama usajili wa Fadlu utagundua jamaa anahitahi watu wa kazi “Ready-made” ambao wamecheza mechi nyingi zenye pressure,Fadlu hataki kujaribu kwa vijana wadogo anataka watu wenye uzoefu ili waje kupiga kazi siyo kujifunza.
Mfano Rushine De Reuck ana miaka 29,Neo Maema ana miaka (29),Jonathan Sowah (25),Khadim Diaw (26) na Alassane Kanté (24).
Guys hapo hakuna mtoto,hao wote wana uzoefu wa kucheza ligi kubwa Africa.
Lakini wengi wao Fadlu amewahi kufanya nao kazi na wengine kama Sowah anawafahamu kwani msimu jana alicheza dhidi yao.