KLABU ya Simba imemtambulisha kiungo Msenegal, Alassane Maodo Kanté (24) kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao akitokea CA Bizertin ya Tunisia.
Kante ni mchezaji aliyeibukia katika klabu ya US Gorée ya kwao, Senegal mwaka 2019 kabla ya kwenda CA Bizertin mwaka 2022.
Anakuwa mchezaji mpya wa pili kutambulishwa rasmi Simba SC baada ya beki wa kati wa Kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck (29) anayeweza pia kucheza kama kiungo wa ulinzi pia kutoka Mamelodi Sundowns ya kwao.
Lakini tayari imethibitika pia Simba SC imekamilisha usajili wa mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah kutoka Singida Black Stars.