Beki wa timu ya Taifa la Tanzania Israel Patrick Mwenda amesaini mkataba wa miaka mitatu na Klabu ya Young Africans baada ya makubaliano ya pande zote tatu. (Singida Black Stars, Young Africans na Mchezaji mwenyewe).
Mwenda sasa atawatumikia wananchi kwa muda wa miaka mitatu kuanzia msimu ujao mpaka 2028.
Yanga wanaimarisha kikosi chao licha ya kuwa na Yao Atohoula na Kibwana Shomari ambapo pia wanaweza kucheza katika eneo hilo.
Mwenda aliwahi kupita kunako vilabu vya Simba Sc, KMC na Singida Black Stars.