KIUNGO wa Kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho (31) ameaga kwenye Yanga SC na kufurahia alioyovuna akiwa na timu hiyo yenye maskani yake makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Aucho amewashukuru na kuwaaga Yanga akijivunia kushinda mataji na klabu hiyo na pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Afrika – ikiwemo kufika Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu wa 2022-2023.
“Young Africans! Familia yangu pendwa, nataka kusema kwamba wakati umefika wa kufunga ukurasa usiosahaulika maishani mwangu. Zaidi ya misimu minne iliyopita nimepata uzoefu wa hisia kali, kufikia malengo ya ajabu na kujenga kumbukumbu isiyofutika nanyi nyote,”amesema Aucho.