Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na klabu ya Yanga SC, Mbrazil Marcio Maximo anatarajia kuwasili nchini kwa ajili ya kujiunga na timu ya KMC ya Kinondoni.
Maximo baada ya kusaini mkataba wa kuinoa timu hiyo, ataungana na wachezaji wa timu hiyo kuelekea Zanzibar ambapo wataweka kambi.
Maximo ataungana na kocha wake msaidizi, kwa vyovyote ushindani kwenye ligi yetu msimu ujao utakuwa mkubwa sana kutokana na uwepo wa makocha wakubwa.