KLABU ya Yanga imemtambulisha kiungo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia, Nizar Abubakar Othman ‘Ninju’ kutoka JKU ya Zanzibar kuwa mchezaji wake mpya kuelekea msimu ujao.
Anakuwa mchezaji mpya wa tano Yanga SC na wa pili tu wa kigeni baada ya viungo Lassine Kouma kutoka Stade Malien ya kwao, Mali na Mguinea, Balla Mousa Conte kutoka CS Sfaxien ya Tunisia.
Wengine ni wazawa wawili kiungo Abdulnasir Mohamed Abdallah kutoka Mlandege ya Zanzibar na winga Offen Francis Chikola kutoka Tabora United.
Aidha, Yanga pia imeajiri kocha mpya Mkuu, Mfaransa Romain Folz mwenye asili ya Morocco ambaye amekuja na Msaidizi mmoja, Kocha wa Makipa. Majdi Mnasria.