Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga SC, Jean Baleke, amefunguka na kusema wazi kuwa anajutia uamuzi wa kujiunga na klabu hiyo, huku akidai kuwa chaguo lake la kwanza alipoondoka Simba, lilikuwa ni Azam FC.
:
Baleke amesema kuwa wakati anafanya maamuzi ya mustakabali wake kisoka, moyo wake ulikuwa unamtuma kwenda Azam kutokana na mazingira na maono ya timu hiyo, lakini hali ya ushawishi kutoka Yanga yalimvuta na kumfanya abadili maamuzi.
:
“Nikikumbuka namna mambo yalivyokwenda, najuta. Azam walikuwa na mpango mzuri na walinionesha heshima ya kipekee, lakini nilishawishiwa kwenda Yanga na sasa naona sikufanya maamuzi sahihi,” alisema Baleke.
:
Kwa sasa haijafahamika wazi Baleke atatua wapi baada ya kuachana na Yanga, lakini taarifa zinadai kuwa Azam bado wanaweza kuwa na nia ya kumrejesha mezani kwa mazungumzo.