TIMU ya taifa ya Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Senegal ‘Simba wa Teranga’ katika mchezo wa mwisho wa michuano maalum ya Baraza la Vyama Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) jioni ya leo Uwanja wa Karatu, Karatu Jijini Arusha.
Mabao ya Taifa Stars yamefungwa na kiungo mshambuliaji wa Azam FC Abdul Suleiman Hamisi ‘Sopu’ dakika ya 52 na beki Ibrahim Hamad Abdullah ‘Bacca’ wa Yanga SC dakika ya 56 baada ya mshambuliaji wa AS Kaffrine, Mapathé Mbodji kuanza kwafungia Simba wa Teranga dakika ya nane.
Kwa matokeo hayo, Taifa Stars inakuwa mshindi wa jumla wa michuano hiyo kufuatia kuifunga na Uganda ‘The Cranes’ 1-0 katika mchezo wa kwanza, timu hiyo iliichapa Senegal 2-1 nayo kwenye mchezo wake wa kwanza hapo hapo Uwanja wa Karatu.