Imefahamika kwamba kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Feisal Salum au Feitoto anatarajia kuvunja mkataba wake na klabu yake ya Azam FC Ili aweze kujiunga na Simba kwa ajili ya msimu ujao.
Ni ngumu kwa Feitoto kujiunga na Simba bila kuvunja mkataba kwa sababu Yanga SC wanataka walipwe bilioni 1 endapo mchezaji huyo akijiunga na Simba kwakuwa maelewano yao na Yanga wakati wanauziana ulieleza hivyo kwamba Feitoto akiuzwa kwa Simba basi Yanga watalipwa bilioni moja.
Tayari mwanasheria wa Feitoto ameanza kuchukua hatua na muda wowote mkataba wake na Azam FC utavunjwa na itakuwa rahisi kujiunga na Simba bure pasipo kuilipa Yanga hata senti tano.