Na Prince Hoza Matua WANAYANGA wanataka timu yao icheze mpira wa kupigiana pasi fupi fupi kwa staili ya kwenda mbele, hawataki mpira wa taratibu na kupigiana pasi za kurudi nyuma, wameshazoeshwa na makocha wao waliopita. Tunajua kabisa kwamba Wanayanga kupata ushindi kwao sio habari ngeni, wamezoeshwa na makocha waliopita, Yanga kushinda makombe ni jadi yao wala sio kitu kigeni, vitu ambavyo kwao ni vigeni ni pale timu yao inafungwa au kutoka sare. Kwa kifupi mashabiki wa Yanga sio watu wa mpira, hawajui kanuni za mpira, kwamba kuna matokeo aina tatu tu, kufungwa, kushinda na kutoka sare, lakini mashabiki wa Yanga wanajua tokeo moja tu la kushinda. Ikitokea timu yao imetoka sare, kocha ananyooshewa kidole, kama sare ya kwanza wanamvumilia kama ya pili wanampa kalipio kali na kama ya tatu wanamfungashia virago, kwa kifupi hawataki matokeo ya aina mbili yatokee. Lakini kwa sasa mashabiki wa Yanga wamebadilika kidogo, kushinda wamegeuza kama asilia yao, ila wanataka timu yao icheze kwa ku...