BAO la kiungo mshambuliaji, Saleh Karabaka dakika ya 90’+4 limeisaidia JKT Tanzania kupata sare ya 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar e Salaam.
Ilikuwa mechi tamu ya funga nikufunge, Mbeya City wakitangulia kwa bao la Hamad Majimengi dakika ya 15, kabla ya Paul Peter kuisawazishia JKT Tanzania – lakini Vitalis Mayanga akaifungia timu kutoka mkoa wa Mbeya bao la pili dakika ya 75 kabla ya Karabaka kusawazisha.
Kwa matoke ohayo, Mbeya City inafikisha point inane katika mchezo wa sita na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi moja zaidi ya JKT Tanzania ambayo pia ina mechi moja mkononi.