Timu ya Singida Black Stars ya Tanzania bara imefanikiwa kutinga hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuiondosha Flambeau du Centre Bujumbura ya Burundi kwa mabao 3-1.
Mchezo huo uliofanyika uwanja wa Azam Complex jijini Dar es Salaam, wageni Flambeau walitangulia kupata bao kupitia kwa David Irishura dakika ya 26 kabla ya Muaku kuisawazishia Singida Black Stars dakika ya 55 na baadaye Clatous Chama kuongeza bao la pili dakika ya 67 wakati dakika ya 72 Idrissa Diomande kufunga bao la tatu.
Jumla Singida Black Stars inatinga makundi kwa mabao 4-2.