Mota Maria ni kocha mwenye uzoefu barani Afrika na Asia, ambapo amewahi kuzinoa timu kama Al Hilal Omdurman ya Sudan na Al Hussein SC ya Jordan.
Anatambulika kwa mbinu ya kucheza soka la pasi chini (ground football), akisisitiza umiliki wa mpira na nidhamu ya kiufundi uwanjani.
Mota Maria alizaliwa Septemba 16, 1966, na aliwahi kucheza kama beki. Alipitia katika vikosi vya vijana vya FC Barreirense na Sporting CP. Alistaafu soka mwaka 2000.
Mfumo wake pendwa kiwanjani ni 4 - 2 - 3 - 1 mfumo ambao hata Yanga wameutumia kwa miaka mitano mfululizo
Kwa sasa, anahudumu kama kocha wa Saham Club nchini Oman. Wakati huu anahusishwa kujiunga na Young Africans Sports Club kuja kuziba nafasi ya Romain Folz