Klabu ya Wydad Casablanca imemtambulisha Kiungo Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Hakim Ziyech ambaye amejiunga na Klabu hiyo kwa Mkataba wa Mwaka mmoja.
Ziyech ameonesha kufurahishwa na kujiunga na miamba hiyo baada ya kukaa nje ya Uwanja kwa mda wa miezi minne na leo ataanza mazoezi rasmi na Wydad.
.
Safu ya Ushambuliaji ya Wydad huenda ikabadilika kutokana na ujio wa Supa Staa huyo ambapo inaweza kuongozwa na Amrabat, Lorch, Aziz Ki na Hakim Ziyech