Klabu ya Yanga Sc imetangaza kumteua aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Angola, Pedro Gonçalves kuwa kocha mkuu mpya klabuni hapo akichukua mikoba ya Roman Folz aliyetupiwa virago.
Gonçalves (49) raia wa Ureno amewahi pia kufanya kazi kama kocha wa kikosi cha vijana wa klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno.