Hii inaweza kuwa taarifa mbaya kwa mashabiki wa Yanga, baada ya mshambuliaji wa kikosi hicho, Clement Mzize, juzi kujitonesha jeraha la goti.
.
Taarifa kutoka kwa Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amesema Mzize amewatia hofu tena kwani juzi jioni katika mazoezi ya mwisho kuelekea kuikabili Silver Strikers, alijitonesha jeraha lake la goti ambalo awali ilielezwa amepona
.
Kamwe amesema kwa Sasa kilichosalia ni Mzize kufanyiwa Vipimo Kisha kujua ukubwa wa Majeraha yake.