Kocha raia wa Burundi Étienne Ndayiragije amekatisha Mkataba Wake na Police FC ya Nchini Kenya Baada ya kuifundisha klabu hiyo kwa Miezi 11.
Étienne Ndayiragije alijiunga na Klabu hiyo Mwishoni Mwa Mwezi Novemba ambapo aliikuta ikiwa nafasi ya mwisho katika michezo nane iliyokuwa imecheza kwenye Ligi Kuu ya Kenya.
Kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo ilishinda Kombe la Ligi Kuu Kenya na kuiwakilisha nchi katika Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika.
Katika Michuano ya klabu Bingwa Afrika, walitolewa na Al Hilal SC ya Sudan katika raundi ya pili.
Inaelezwa kuwa Étienne Ndayiragije kuna timu ambayo iko inawinda saini yake ili aweze kuwa Kocha Mkuu ingawa bado haijawekwa wazi ni Klabu ipi.
