Na Mwandishi Wetu
MSANII wa kike wa muziki wa kizaxi kipya anayejulikana kwa jina la Naina D, ambaye pia anatamba na wimbo wake uitwao "Nipe tamu", ametambulisha wimbo wake mpya uitwao Serious.
Akizungumza na Mambo Uwanjani Blog, Naina D amedai kwamba wimbo wake mpya aliourekodi kwa njia ya audio, unaelimisha jamii na kuburudisha.
"Wimbo ni wa mapenzi na unalenga kumpata mtu aliye- serious na si wa kupotezeana muda", alisema na kuongeza.
Wimbo huo ameutambulisha kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo youtube, facebook, TikTok, pia atautambulisha kwenye stesheni za redio.