Kikosi cha wachezaji 23 cha Silver Strikers kimeondoka nchini Malawi hii leo kuja Jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya mchezo wa pili wa mtoano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga SC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Silver Strickers walipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa kwanza ambapo inahitaji sare yoyote Ili kutinga makundi.