TIMU ya JKT Queens ya Tanzania imepangwa Kundi B pamoja na mabingwa watetezi, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ASEC Mimosas ya Ivory Coast na Gaborone United ya Eswatini katika Ligi ya Mabingwa Wanawake Afrika 2025.
Katika droo iliyopangwa leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Jijini Cairo nchini Misri – mabingwa mara nyingi wa michuano hiyo,
Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wenye mataji mawili wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji, FC Masar, AS FAR Rabat ya Morocco, Primiero de Agosto ya Angola na US FAS Bamako ya Mali.
Michuano hiyo ya tano ya Ligi ya Mabingwa ya Wanawake Afrika inatarajiwa kufanyika nchini Misri kuanzia Novemba 8 hadi 21 mwaka huu ikishirikisha timu hizo nane zilizogawanywa katika makundi mawili.

