KLABU ya Azam FC imeamua kuutumia Uwanja wa New Amaan Complex kwa ajili ya mechi zake za hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika baada ya Uwanja wao wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
“Mashabiki wetu na wakazi wa Zanzibar kwa ujumla tunawaletea burudani ya mechi zetu za Kombe la Shirikisho Afrika zilizobakia kwa msimu huu 2025/26, baada ya kuuchagua Uwanja wa New Amaan Complex kama uwanja wetu wa nyumbani,” imesema taarifa ya Azam FC leo na kuongeza; “Zanzibar tunakuja kuanzia hatua ya makundi, kaeni tayari kutupokea! Hii ni zamu ya Azam.
