Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2025

Ayoub Lakred atambulishwa FUS Rabat

Golikipa wa Simba SC Ayoub Lakred amejiunga na FUS Rabat kwa mkataba wa miaka miwili. Kipa huyo kutoka Morocco aliagana na Simba, na tayari amerejea nyumbani kwao Morocco. Mkataba wake na FUS Rabat umesainiwa leo rasmi asubui

Singida Black Stars yapigwa changa la macho

Klabu ya Singida Black Stars imeshangazwa na taarifa za MVP wa Ligi Kuu ya Burkina Faso Raouf Memel Dao (21) kutambulishwa na klabu ya APR. Tayari Dao alikuwa amesaini mkataba na Singida Black Stars lakini ghafla ameibukia APR. Baada ya kutangazwa na APR wakala wake Salome Compaoré ameshangazwa huku akisema mteja wake tayari alishasaini Singida Black Stars.

Injinia Hersi kuendelea kuongoza Yanga hata alipata ubunge

Rais wa klabu Yanga injinia Hersi Said ameeleza kuwa ataendelea na uongozi wake ndani ya klabu Yanga huku akiwa na majukumu mengine ya kugombania uongozi katika wilaya ya Kigamboni Mbali na hapo Hersi Said ameeleza kuwa makao Rais wa klabu ya Yanga Arafat Haji ataendelea kutumikia uongozi ndani ya klabu Yanga wakiwa pamoja

Picha: Gwaride la Yanga.....

Mabingwa wa Ligi Kuu bara, Ngao ya Jamii na kombe la CRDB, Yanga SC wameanza kupiga gwaride lao hii leo likiwa ni maadhimisho ya kusherehekea Mataji yao matano. Mbali ya kushinda Mataji matatu, Yanga wameshinda kombe la Toyota na kombe la Muungano.

Seleman Bwenzi aitosa Coastal Union na kujiunga Mashujaa FC

Baada ya uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga kusuasua kumnunua kiungo mshambuliaji wa KenGold ya Chunya mkoani Mbeya, Seleman Bwenzi, hatimaye Mashujaa FC ya Kigoma imefanya kweli-. Mashujaa FC inayonolewa na Salum Mayanga, imeamua kuingilia kati dili la Bwenzi na kuvunja benki na kumsajili kiungo huyo mshambuliaji aliyefanya vizuri akiwa na timu hiyo iliyoshuka daraja. Bwenzi sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa FC msimu ujao.

Duke Abuye huyooo Algeria

Licha ya kufanya vizuri kwenye michezo miwili dhidi ya Simba na Singida Black Stars, Duke Abuye anatarajia kuondoka Jangwani na msimu ujao ataonekana nchini Algeria. Kiungo huyo aliyecheza vizuri zaidi kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo akiziba vema nafasi ya Khalid Aucho huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 na jana akicheza vizuri dhidi ya Singida huku Yanga ikishinda tena mabao 2-0 na yeye akifunga bao la kwanza dakika ya 39. Mkataba wake wa mkopo alitokea Polisi ya Kenya ingawa Yanga alitua akitokea Singida Black Stars, tayari klabu ya JS Kaybilie ya Algeria imeshamalizana na Polisi na kinachosubiriwa na kumalizika kwa shughuri za kufunga msimu na Yanga ikiwa imeshinda Mataji matano msimu huu.

Mbeya City yaibomoa Yanga

Klabu ya Mbeya City ya jijini mbeya ipo katika mazungumzo na Winga wa Klabu ya Yanga SC, Faridi Musa , ambae tayari mkataba wake upo ukingoni kumalizika katika Klabu ya Yanga SC. Faridi Musa amekuwa na nafasi finyu katika Kikosi cha Yanga msimu uliomalizika jambo ambalo limemfanya kupoteza nafasi kabisa katika Kikosi cha Yanga SC. Mbaya City ambayo imepanda ligi msimu huu tayari wameanza kufanya usajili kwenye Kikosi chao ili kuifanya Klabu hiyo Kuwa na msimu mzuri ujao kwenye ligi kuu Tanzania bara.

Yanga yatwaa kombe la CRDB Cup 2024/2025

Mabingwa wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu wametwaa kombe la CRDB Cup 2024/2025 baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar. Dakika ya 39 kiungo mkabaji Duke Abuye raia wa Kenya alitangulia kwa kuipatia bao Yanga kabla ya Clement Francis Walid Mzize kuandika bao la pili dakika ya 49. Hata hivyo mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah raia wa Ghana alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 86 na mwamuzi Ahmed Arajiga. Huu ni ubingwa wa nne mfululizo kwa Yanga kwenye kombe hilo historia ambayo wameiandika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa michuano hiyo na pia kwa hapa nchini kuwa timu ya kwanza kutwaa mara nne mfululizo. Ikiwa katika msimu huu imetwaa makombe matano ambayo ni pamoja na kombe la TUYOTA, Muungano, Ngao ya Jamii na Ligi Kuu bara.

PSG yatinga robo fainali kombe la Dunia la vilabu

TIMU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa imefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Inter Miami CF usiku huu Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia. Mabao ya mabingwa hao wa Ulaya, PSG yamefungwa na kiungo Mreno, João Neves mawili, dakika ya sita na 39, Mabeki, Muargentina Tomás ‘Toto’ Avilés aliyejifunga dakika ya 44 na Mmorocco, Achraf Hakimi dakika ya 45+3.

Fabrice Ngoma awaaga Wanasimba

Kiungo wa Simba SC, Fabrice Luamba Ngoma amewaandikia ujumbe viongozi, mashabiki na timu nzima ya Simba SC, huku akiwakumbusha kuendelea kuiunga mkono klabu hiyo yenye maskani yake mitaa ya Msimbazi Kariakoo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ngoma ameandika: “Namshukuru kila mmoja ambaye alinifanya mimi kujisikia nipo nyumbani nikiwa Simba. Shukrani zangu ziende kwa Salim Abdallah ‘Try Again’ na Boss MO ambao walinileta mimi misimu miwili iliyopita. Shukrani kwa kocha, wafanyakazi na wachezaji ambapo kwa pamoja tulishirikiana katika chumba cha kubadilishia jezi. Hatujaweza kuyafikia baadhi ya malengo yetu, lakini kumbukumbu zitasalia akilini mwangu na moyoni. Kwenu mashabiki wa Simba, ahsanteni kwa ushirikiano, msiiache hii timu, nyakati nzuri zinakuja hasa kwa kupitia kocha kama Fadlu. Ahsanteni na kila la kheri” ameandika Ngoma

Aziz Ki kurejea Yanga baada ya mkopo kuisha

Stephanie Aziz Ki alijiunga na Wydad kwa mkopo mfupi wenye kipengele cha kununuliwa mazima kabla ya tarehe 10/07/2025. Makubaliano ya Yanga na Wydad ni kulipwa pesa ya usajili wa Aziz (signing fee) ya Tsh 1.7b kabla ya tarehe 10/07/2025 lah sivyo Aziz atarejea nchini. Wydad na Aziz Ki walihitajiana sana kuelekea FIFA Club world Cup hivyo ikabidi kiwekwe kipengele cha kulipa pesa hiyo kabla ya tarehe 10 endapo watalidhika na kiwango chake. Kisheria Aziz bado ni mchezaji wa Yanga ndiyo maana bado hajaondoa “Profile Picture” ya Yanga kwenye Instagram yake,unless Wydad wamalizane na Yanga kabla ya july 10.

Debora Mavambo atupiwa virago Simba

Simba Sports Club imeachana rasmi na kiungo wao raia wa Congo Brazzaville, Debora Mavambo, baada ya muda mfupi wa kuitumikia klabu hiyo. Hatua hii ni sehemu ya mabadiliko makubwa yanayotarajiwa ndani ya kikosi cha Simba kwenye dirisha hili la usajili, ambapo taarifa zinaeleza kuwa wachezaji wengine watakaoachwa watajulishwa hibi karibuni. Mavambo alijiunga kama kiungo mwenye matumaini, lakini safari yake imefikia ukomo kabla ya msimu mpya wa 2025/26.

Arajiga kupuliza filimbi fainali ya CRDB leo

REFA Ahmed Arajiga wa Manyara ndiye atakayechezesha Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB kesho baina ya Yanga SC ya Dar es Salaam na Singida Black Stars ya Singida kuanzia Saa 2:00 usiku Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Arajiga atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Hamdani Said wa Mtwara watakaokuwa wakikimbia na vibendera pembezoni mwa Uwanja, wakati refa wa nne mezani atakuwa ni Tatu Malogo wa Tanga, Kamishna Zakayo Mjema wa Arusha na Mtathmini wa Marefa, Victor Mwandike wa Mtwara. Yanga SC kesho wanataka kumalizia msimu mzuri katika mashindano kwa kutwaa taji la nne baada ya Ngao ya Jamii, Kombe la Muungano na Ligi Kuu na la tano kwa ujumla pamoja na Kombe la Toyota nchini Afrika Kusini, michuano ambayo ilishirikisha timu za Augsburg ya Ujerumani na wenyeji, TS Galaxy na Kaizer Chiefs. Kwa Singida Black Stars watakuwa wanataka kushinda taji la kwanza kabisa katika historia yao, wakiwa na kumbukumbu ya kulikosa ...

Azam FC yakubali yaishe kwa Gibril Sillah Yanga

KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na winga wake Mgambia, Gibril Sillah (26) baada ya misimu miwili ya kuwa na timu hiyo kwa misimu miwili na nusu. Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Azam FC imemuaga na kumshukuru Sillah ambaye naye pia kwenye kurasa zake amefanya hivyo. Kwa mujibu wa Azam FC, katika kipindi cha misimu miwili na nusu, Sillah amecheza jumla ya mechi 68 akifunga mabao 21 na kutoa pasi za mabao 10 yaliyofungwa na wengine. Sillah ameandika kuishukuru Azam FC akisema; “Asanteni Azam Football Club kwa yote mliyonifanyia katika kipindi hiki cha miaka miwili,”.

Yamal ashangaza kisiwa cha Ibiza

Supastaa wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17, Lamine Yamal hivi majuzi ameshangaza watu wakati wa mapumziko yake ya msimu huu wa joto kwenye Kisiwa cha Ibiza (Hispania). Yamal alinaswa akiwa likizoni kwenye boti ya kifahari huko Ibiza kwa gharama ya kukodisha inayokadiriwa kuwa euro 5,000 sawa na milioni 15 za kitanzania kwa siku, ambapo Kwenye boti hiyo, alienda marafiki zake pamoja na wasichana wachanga wapatao 8 ambao aliwaalika kufurahia nao. Picha kutoka kwenye boti hiyo zinaonesha Yamal akiwa hana shati, akipiga picha na wasichana hao waliovalia bikini, zimesababisha taharuki mtandaoni. Watu wengi wakionesha kushangazwa na kutilia shaka maisha ya anasa ya mwanasoka huyo mchanga. Bila shaka, Yamal yuko kwenye likizo ya majira ya joto na anaweza kufurahia atakavyo kabla ya kurudi uwanjani msimu ujao. Lakini mashabiki wengi hawawezi kujizuia kuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa staa huyu wa soka, hasa wanapomlinganisha na kizazi cha mfano cha Messi, Iniesta.

Yanga yamwekea pingamizi Karia

Young Africans Sc imemuwekea pingamizi Rais wa TFF Wallace Karia na pingamizi hilo limewasilishwa ofisi za TFF saa 9:30 Alasiri ya leo likiwa limesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wao (CEO) Andre Ntine. Yanga SC katika pingamizi lao wanaitaka Kamati ya Uchaguzi chini ya Mwenyekiti wake Wakili Kilomoni Kibamba kumuondoa Karia katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi wakiwa na hoja Kuu 3 . 1. Matumizi mabaya ya madaraka kwa kuchukua endorsement 46 Kati ya 47 2. Kuanza kampeni kabla ya muda kwa kukusanya endorsement 46 kabla ya tangazo la Uchaguzi kutolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF. 3. Wanapinga Karia kugombea mara ya 3 wakisema ni kinyume na sera ya michezo nchini ambayo inataka vyama vya michezo viongozi wake kukaa madarakani kwa vipindi 3 vya miaka mitatu mitatu au vipindi 2 vya miaka minne minne. .

CS Sfaxien yakataa mamilioni ya Scotland kumuuza Balla Moussa Conte

Klabu ya CS Sfaxien imekataa ofa ya USD 200K (Tshs Milioni 521) kutoka Hibernian FC ya nchini Scotland ikihitaji saini ya Kiungo Balla Moussa Conte (21) CS Sfaxien wanahitaji USD 2M (Tshs Bilioni 5.2) ili kumuachia mchezaji huyo katika dirisha lijalo la uhamisho na CS Sfaxien ina amini klabu hiyo ya Scotland itaboresha ofa yake kwa wakati ujao Simba SC pia inamfatilia kiungo Balla Moussa Conte kuelekea msimu ujao ili kuongeza nguvu na mkataba wa Balla Moussa Conte na CS Sfaxien unamalizika mwaka 2026.

Mtoto wa JPM achukua fomu ya kugombea ubunge viti maalum

Jesca Magufuli ambaye ni Mtoto wa Rais wa awamu ya tano Hayati Dr. John Pombe Magufuli, leo June 28 2025 amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum kupitia Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Taifa. Jesca ni Binti ambaye amejipambanua kama sauti ya matumaini kwa Vijana na Wanawake wa Tanzania akisimamia maadili, haki na maendeleo jumuishi ambapo amelenga kupeleka nguvu mpya ya kijana Bungeni, kusimamia ajenda za maendeleo kwa Vijana, Wanawake na Jamii kwa ujumla huku akihakikisha UVCCM inasikika, inaonekana na inawakilishwa kwa heshima katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. “Nipo tayari kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu, umoja na kwa kutanguliza maslahi ya Vijana na Wanawake, Geita inapeleka sauti ya mabadiliko chanya,” amesema Jesca Magufuli mara baada ya kuchukua fomu hiyo leo.

Les Aigles du Congo mabingwa wapya DRC

TIMU ya FC Les Aigles du Congo (Eagles of Congo) ya Kinshasa imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ijulikanayo kama Linafoot kwa mara ya kwanza katika historia yake baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na TP Mazembe Ijumaa ya jana (Juni 27, 2025) Uwanja wa Kamalondo, Lubumbashi. Beki Heltone Kayembe alianza kuifungia Aigle du Congo ‘Des Samourais’, (The Samurai) dakika ya 35 akimtungua kipa Baggio Siadi Ngusia, kabla ya Patrick Mwaungulu kuisawazishia TP Mazembe dakika ya 47 akimtungua kipa Nathan Dibu kufuatia kazi nzuri ya Patient Mwamba. Kwa matokeo hayo, Aigles du Congo inayofundishwa na Kocha wa zamani wa Tabora United, Anicet Kiazayidi inamaliza na pointi 35 kileleni mwa Linafoot ikifuatiwa na FC Saint Eloi Lupopo ya Lubumbashi pia yenye pointi 33 baada ya mechi 16 kwenye ligi ya timu 12 na zote zinafuzu Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao. Timu ya AS Maniema iliyomaliza nafasi ya tatu kwa pointi zake 32 inakwenda Kombe la Shirikisho ...

Injinia Hersi, Arafat wajitosa kuwania ubunge

Rais wa klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said na Makamu wake Arafat Haji wote wawili wamejitosa kwenye ulingo wa siasa na watagombea ubunge. Tayari Injinia Hersi amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM wakati Arafat anatarajia kuchukua fomu kwenye Jimbo la Shaurimoyo, Zanzibar. Hii yote inatokana na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwanamichezo hivyo wanamichezo wengi wameamua kujitosa kwenye majimbo kuwania ubunge.

CAF yatangaza kanuni mpya Ligi ya mabingwa Afrika

CAF imetangaza kanuni kuu kabla ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho msimu wa 2025/26: Julai 31: Tarehe ya mwisho kwa mashirikisho ya wanachama kuwasilisha vilabu vitakavyoshiriki Vilabu vinaweza kusajili wachezaji hadi 40 Substitution 5 kwa kila mechi | Wachezaji 9 benchi Wachezaji wapya waliopatikana kwenye dirisha la usajili la Januari lazima wasajiliwe saa 72 kabla ya mechi ili waweze kucheza 🇩🇿🇦🇴🇨🇮🇪🇬🇱🇾🇲🇦🇳🇬🇨🇩🇿🇦🇸🇩🇹🇳🇹🇿 Nchi 12 zenye nafasi ya kuingiza vilabu viwili kwa kila mashindano: Aljeria, Angola, Côte d’Ivoire, Misri, Libya, Morocco, Nigeria, DR Congo, Afrika Kusini, Sudan, Tunisia, na Tanzania.

Sowah awapiga mkwara Yanga

Mshambuliaji wa Singida Black Stars, Jonathan Sowah raia wa Ghana, ameipiga mkwara Yanga kwamba kama wakifanya makosa keshokutwa katika mchezo wa fainali atawaadhibu. "Simba na Yanga hazina tofauti... kama ambavyo Simba walifanya makosa nikawafunga, vivyo hivyo Yanga wakifanya makosa nitawafunga" Jonathan Sowah, straika wa Singida Black Stars....kuelekea fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB

Ngoma akataa kusaini mwaka mmoja Simba

Klabu ya Simba SC imempa ofa ya kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kiungo Fabrice Ngoma (31) kuelekea msimu ujao Ngoma amekataa ofa hiyo na anahitaji mkataba mpya wa miaka miwili ikiwa kinyume na matakwa yake ataondoka dirisha kubwa lijalo la uhamisho Simba SC ina nia ya kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja tu na mpaka sasa bado hakuna hatima baina ya pande zote mbili

Simba yaanza na Morice Abraham

Kiungo fundi Morice Abraham amejiunga na simba sc kwa mkataba wa miaka miwili, Kiungo huyo mshambuliaji siku za hivi karibuni akifanya mazoezi na simba baada ya kuachana na club ya Fk spartak subotica ya Serbia, Kocha fadlu ameridhika na uwezo wake na rasmi sasa ni mchezaji wa simba sc,

Ahmed Ally aifananisha Simba na Real Madrid

“Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBC. Wana Simba tuepuke presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani. Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31 Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na Dkk 45 za Kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu. Points tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita. Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu. Si mara ya kwanza Simba kukaa miaka minne bila Ubingwa, tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka Minne mfululizo. Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau. Madrid amepote...

Yanga yaanza tizi Zanzibar kuiwinda Singida Black Stars keshokutwa

Kikosi cha Yanga SC baada ya kufika leo Zanzibar kimeanza mazoezi yake rasmi kujiandaa na Mchezo wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Nchini Tanzania dhidi ya Singida Black Stars ambapo mchezo huo utachezwa jumapili ya wiki hii

Yanga yazipiga bao Simba, Azam kumnasa MVP wa Ivory Coast

Uongozi wa klabu ya. Yanga upo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ivory Coast, Célestin Ecua(23) Celestin Ecua akiwa na Kikosi cha Asec Mimosas amefunga Mabao (15) na kutoa pasi za usadizi (Assist) 12 . Ndiyo (MVP) wa ligi kuu ya Ivory Coast. alikuwa anakipiga kwa mkopo Asec akitokea Zoman Fc. Jama ni fundi sana anauwezo wa ku dribble ku funga ku assist ana speed na nguvu pia, anacheza namba 10 pia anaweza kucheza kama winger Célestin Ecua anakuja kuchukua nafasi ya Stephan Aziz ki kama mambo yataenda sawa.

Mashabiki wa Yanga, Simba waungana kunywa supu ya Ngamia kusherehekea ubingwa wa Yanga

Mashabiki wa Klabu ya Yanga pamoja na wale wa Simba waliungana pamoja kusherehekea Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo Yanga walibeba hapo juzi na kwenye sherehe hizo Yanga waliandaa Supu ya Ngamia. . Yanga walibeba Ubingwa huo kwa kumfunga Mtani wake, Simba SC bao 2-0.