Baada ya uongozi wa klabu ya Coastal Union ya Tanga kusuasua kumnunua kiungo mshambuliaji wa KenGold ya Chunya mkoani Mbeya, Seleman Bwenzi, hatimaye Mashujaa FC ya Kigoma imefanya kweli-.
Mashujaa FC inayonolewa na Salum Mayanga, imeamua kuingilia kati dili la Bwenzi na kuvunja benki na kumsajili kiungo huyo mshambuliaji aliyefanya vizuri akiwa na timu hiyo iliyoshuka daraja.
Bwenzi sasa atakuwa sehemu ya kikosi cha Mashujaa FC msimu ujao.