Klabu ya Singida Black Stars imeshangazwa na taarifa za MVP wa Ligi Kuu ya Burkina Faso Raouf Memel Dao (21) kutambulishwa na klabu ya APR.
Tayari Dao alikuwa amesaini mkataba na Singida Black Stars lakini ghafla ameibukia APR.
Baada ya kutangazwa na APR wakala wake Salome Compaoré ameshangazwa huku akisema mteja wake tayari alishasaini Singida Black Stars.